Monday, September 24, 2012

MIGOMO KWELI NDO SULUHU YA HAKI ILIANZIA MAREKANI SASAHIVI NI KENYA WALIMU WAPATA NYONGEZA YA ASILIMIA MIATATU YA MSHAHARA

Kwa mara ya kwanza serikali ya Kenya imekubali kutoa nyongeza ya asili mia 300 kwa mishahara ya walimu ambao wamekuwa katika mgomo wa kitaifa kwa wiki tatu sasa.

Kutokana na maafikiano hayo kati ya serikali na chama cha walimu nchini KNUT, sasa walimu wanatarajiwa kurejea kazini Jumatatu. Hatua hiyo sasa itawapa afueni maelfu ya wanafunzi hususan wa shule za msingi na upili za umma ambao hawajafunzwa wakati huu walimu walipokuwa mgomoni.

Vyama vya walimu nchini Kenya KNUT na Kuppet vilikuwa vikishinikiza serikali kuwalipa walimu nyongeza hiyo kwa awamu moja. Awali serikali ya Kenya ilikuwa imekataa kutekeleza matakwa hayo na kuwataka walimu kukubali kulipwa kwa awamu tatu, awamu ya kwanza ikitekelezwa Oktoba mwaka huu.

Mwalimu wa chini aliyekuwa akipata shilingi 13,000 sasa atapata shilingi 39.000. Serikali ya Kenya imetenga zaidi ya dola 159 milioni kuwalipa zaidi ya walimu 250,000 ambao walikuwa wakigoma kulalamikia mishahara duni na mazingira mabaya ya kazi.

via BBC Swahili