Mbunge wa Viti maalum Chadema Mh, Filipa Mturano akiwa akiuliza swali kuhusu namna ya kuchanganya Kemikali kutoka kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Magnus ambao walikuwa wanasherehekea Mahafali yao ya Tano leo ambao idadi yao ni wanafunzi 75 wavulana 30 na wasichana 45. Mturano alikuwa Mgeni rasmi katika Mahafali hayo ambapo aliahidi kuwatafutia wafadhili wa kusaidia maendeleo katika Shule hiyo yenye changamoto ya ukosefu wa Vitendea kazi katika Chumba cha Computer (Tehama) pamoja na Kukosekana kwa Uzio inayopelekea wanafunzi wengi kutoroka Shule pamoja na Udogo wa Mabweni hasa kwa Wavulana. |