Kuna taarifa nimezipata kutoka kwa mmoja wa makada wa CCM Mkoani Mwanza
kuwa watu 10 wamekamatwa kwa kitendo cha kumzomea Waziri Mkuu Pinda pale
uwanja wa Sahara Jijini Mwanza. Kada huyo ya CCM ameonyeshwa
kusikitishwa na kitendo hicho akisema kuwa kitendo hicho ni uhuni na
kwamba kuzomewa kwa Pinda ni ujumbe unaotakiwa kufanyiwa kazi na CCM na
serikali yake na si kukamata watu.
Nimejaribu kuzungumza na baadhi ya askari polisi jijini Mwanza juu ya
taarifa hizi, wamekiri kwamba juzi watu sita walikuwa wamekamatwa na
polisi kitengo cha intelijensia kwa mahojiano kuhusiana na Pinda
kuzomewa hata hivyo wamesema hawajui kama waliendelea kushikiliwa au
waliachiwa. Aidha nimezungumza na mmoja wa askari wa kitengo hicho yeye
amekanusha vikali habari hizi.
Tufuatilie ili tujue ukweli kisha tujadiri kama ni halali kumkamata mtu
eti kisa kamzomea kiongozi wa serikali kwa kusema hatuitaki CCM! Source Jamii Forum