Sunday, September 23, 2012

MWEKEZAJI ALAANI KITENDO CHA YEYE KUTISHIWA KUFUNGIWA KIWANDA CHAKE BILA MAKOSA



Mkurugenzi wa Kiwanda cha TASIPA kinachotengeneza Viroba Bw, Lain Ding, akiongea na waandishi wa habari juu ya Kutaarifiwa kufungiwa kwa Kiwanda chake na mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Heche Sagute ambaye alikuja ofisini kwake na kuacha Bussiness card na kuwaambia kuwa Kiwanda kimefungwa.
Bw, Ding amesema kuwa, sababu za wao kuambiwa wafunge kiwanda ni malalamiko ya wananchi kuwa wao wanatiririsha maji machafu yenye Kemikali katika mto uliopo jirani na Kiwanda chao jambo ambalo Bw, Ding amesema kuwa swala hilo halina ukweli na kwamba wao hawatiririshi maji yenye kemikali yoyote. Baadhi ya waandishi waliokuwemo katika kikao hicho tulishuhudia maji yanayodhaniwa kuwa yanakemikali na kukuta kuwa hayana kemikali zozote.

Ameongeza kuwa, swala la yeye kufungiwa kiwanda hana taarifa nalo na kusema kuwa yeye hawezi kufunga kiwanda mpaka apewe taarifa rasmi ya maandishi.
Meneja msaidizi wa Kiwanda hicho Bw, Simon Haule akionyesha namna kiwanda hicho kinavyosafisha taka chafu za plastic kwa kutumia maji ya asili na yasiyo na kemikali zozote.

Mkazi wa Dar es Salaam akiwa amebeba mzigo wa viroba vilivyotupwa ambavyo vinanunuliwa katika kiwanda hicho

Mfanyakazi wa Kiwanda hicho akionyesha baadhi ya Takataka ambazo zitasafishwa ili ziweze kutengeneza viroba vipya.