Wednesday, September 19, 2012

BAKWATA WALAANI VIKALI FILAMU YA INNOCENCE OF MUSLIM

Sheikh Mkuu wa  Tanzania  Mufti Issa Bin  Shaaban  Simba akisoma tamko la kulaani filamu ya Inocence of Muslim  inayomdhalilisha Mtume Muhamad(S.A.W) mbele ya waandishi wa habari katika makao makuu ya baraza kuu la waislamu nchini Bakwata leo
 
Ameongeza kuwa kutokana na filamu hiyo ni wakati muafaka sasa kwa nchi ya marekani kupitia sheria zake hasa za uhuru wa kujieleza kwa lengo la kuzuia uchochezi na uhasama baina ya watu wengine hususan kwa madhehebu ya dini
Amesema waislamu wa Tanzania hawataweza kuvumilia udhalilishaji unaofanywa mara kwa mara na raia wa marekani dhidi ya uislamu na kutolea mfano matukio ya kuchomwa moto kwa kitabu kitukufu cha Q’uran pamoja na kuandikwa kwa majina ya mwenyezi mungu na mtume katika viatu vya NIKE
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kazini