Mkurugenzi mkuu wa TWAWEZA Bw, Rakesh Rajami |
Mafanikio ya mda mfupi yamefikiwa katika huduma ya afya
Lakini maboresho ya matokeo ya afya ya muda mrefu yahitaji kazi zaidi
Dar es Salaam, 18 Septemba: Mpango wa serikali wa kutoa kipaumbele katika usambazaji wa vyandarua
kwa kaya umepata mafanikio makubwa. Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 95 ya kaya za Dar es
Salaam zinamiliki angalau chandarua kimoja. Matumizi ya vyandarua ni hatua muhimu katika kuzuia
mapambano dhidi ya malaria. Hata hivyo wakati huo huo, zaidi ya nusu ya wakazi wa Dar es Salaam
wametaarifu kuchemsha au kuwekea dawa maji yao kabla ya kunywa. Kwa vile idadi kubwa ya
magonjwa yanayosababishwa na maji yanaweza kuzuiwa kwa kuwekea maji dawa ya klorini au
kuyachemsha.Magonjwa hayo ni pamoja na kipindupindu na homa ya matumbo.Hata hivyo uchache wa
watu wanaokunywa maji safi ni changamoto kwa sekta ya afya kwa umma. Matokeo haya na
mengineyo yameelezwa kwa kina kwenye muhtsari sera uitwao “Wakazi wa Dar wanasemaji kuhusu
afya? Huduma za afya na utendaji katika Dar es Salaam” ambao umetolewa leo.
Muhtsari huu umejikita kwenye utafiti kuhusu utoaji wa huduma kwa umma uliofanywa na Uwazi
iliyoko Twaweza kati ya Agosti na Septemba 2010. Jumla ya kaya 550 zilizochaguliwa kwa nasibu
zilitembelewa na timu ya watafiti katika wilaya za Ilala, Temeke, na Kinondoni. Waliiulizwa kuhusu hali
ya maisha ya wananchi na uzoefu wao wa huduma za umma.
Utafiti huu umeonyesha kuwa hali ya afya inaendelea kuwa changamoto kubwa kwa wakazi wa Dar es
Salaam . Kaya moja katika kila kaya tatu imeripoti kuuguliwa na mtu miongoni mwa wanandugu wa kaya
hiyo katika wiki iliyotangulia utafiti. Cha kuogopesha ni kuwa , moja ya tatu ya kesi zilizoripotiwa
ziliwahusu watoto, ambao mara nyingi wako katika hatari zaidi ya ugonjwa huo. Mafanikio
yaliyopatikana katika hatua za msingi za kuzuia maradhi , kama vile usambazaji wa vyandarua vyenye
dawa, ni hatua muhimu katika kuelekea kupambana na masuala ya afya ya umma. Hata hivyo kiwango
cha watu wasiotumia maji safi kinaashiria tahadhari ya haraka yapaswa kuchukuliwa.
Utafiti zaidi kuhusu matokeo ya vituo vya afya pia umeonyesha baadhi matumaini, lakini kuna baadhi
ya masuala muhimu ambayo bado yanahitaji kushughulikiwa.
Katika kaya ziliripoti kuwa zilikuwa na mgonjwa wiki kabla ya utafiti, asimilia 86 wamearifu
kutafuta tiba katika kituo cha afya. Matumizi haya ya vituo vya afya ni hatua muhimu katika
utambuzi sahihi wa ugonjwa na matibabu yake.
Kuna uhitaji mkubwa wa huduma ya vituo vya afya vya serikali, asilimia 60 ya washiriki
wameaarifu kutumia vituo hivyo kwa ajili ya matibabu. Takwimu hizi zinaongezeka kwa kasi
wakati kiwango cha kipato cha kaya kikihusishwa kwenye mchanganuo . Miongoni mwa kaya
maskini zaidi, asilimia 82 hutumia vituo vya afya vya serikali.