Tuesday, August 7, 2012

WATANZANIA WAFANYA VIZURI NCHINI UJERUMANI

Rais  wa TSC Academy Bw, Hiran Altaf, Akiongea na waadishi wa habari leo jijini Dar es Salaam juu ya Ushindi wa Timu yaTSC Academy nchini Ujerumani. 
 Timu ndogo iliyokwenda kuiwakilisha Tanzania Nchini ujerumani imerudi nchini ikiwa na ushindi wa Nafasi ya Pili. Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa TFF jijini Dar es Salaam Rais wa TSC Academy Bw, Hirani Altaf  ambayo ni moja ya Kampuni iliyoandaa mashindano hayo, alisema kuwa, Baada ya kufika nchini ujerumani Timu yake ilicheza vizuri na hamna Hata timu moja iliyofanikiwa kuifunga timu hiyo yenye vijana wadogo chini ya Umri wa miaka 20. Aidha Bw, Hiran alitumia nafasi hiyo pia kuwashukuru wadhamini wote waliofanikisha Timu hiyo kufika ujrerumani na kurudi na Ushindi wa Nafasi ya Pili.
Mkurugenzi wa TSC  Academy Bw, Mutani Yangwe   akionyesha baadhi ya Vikombe vilivyotwaliwa na Timu hiyo huko Ujerumani na wanao onekana nyuma ni wachezaji walioshiriki katika michezo nchi i Ujerumani.

Naye Mkurugenzi wa TSC Academy alisema kuwa kutokana na Kiwango kilicho onyeshwa na Wachezaji hao, wametokea wadhamini kutoka ujerumani walioamua kujitolea kugaramiamafunzo ya wachezaji watatu kutoka kwenye timu hiyo ambapo Bw, Yangwe aalisema kuwa wachezaji hao watakwenda kupatiwa mafunzo nchini humo.

Mwalimu wa Timu hiyo Bw,Rogashile Kaijage, akisisitiza jambo wakati akiongea na waandishi wa Habari ambapo aliitaka serikali itizame vipaji vidogovidogo vinavyochipukia kwani kuna wachezaji wazuri na wasiotambulika na serikali.