Vitu vyote vilitolewa nje. |
Hapa ana amishia kwa jirani. |
Watu watano wasiojulikana wamevamia kijiji cha Butiama kata
ya Mabwe pande wakiwa na silaa aina ya Bastola (2) ambapo waliwatishia kuwaua
wanakijiji hao na waliwataka wanakijiji
hao waondoke kijijini Hapo kwani hawatakiwi kuishi katika maeneo hayo.
Mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana Steven Franck alisema kuwa
, watu hao walifika kijijini hapo pasipokujulikana wametoka wapi na kuvamia
nyumba ya Bwana mmoja aliyefahamika kwa jina la Cheyo Peter.
Franck alisema kuwa Watu hao ambao hawakuweza kutambulika kwa
Urahisii walikuja na kutaka kuwaondoa wanakijiji wanaoishi maeneo hayo kwa dhana ya kwamba
wanakijiji hao wamevamia maeneo yao, pia
watu hao walimvamia Bwana huyo maarufu kama Mzee Cheyo na kutaka kumfyatulia
Bastola huku wakiwa wanamwambia mke wake
achukue vitu vyake vyote na aondoke
kwani yeye ndiye aliye uza msitu huo.
Alisema baada ya kumvamia bwana cheyo walitoka kwenye nyumba
hiyo na kuwatishia wananchi na ndipo wananchi wakaonganisha nguvu na
kuwanyan’ganya Bunduki hizo na kasha kuziwasilisha katika Ofisi ya Serikali ya
Mtaa iliyopo Mabwepande.
“Tunaiomba serikali itumulike na kututambua sisi wananchi
wake kwani tumekuja huku kutokana na shida ya makazi, na pia tulifwata taratibu
zote kwamba tumekuta Pori na tukafyeka kwa ajili ya kuweka makazi yetu”,alisema
Steven.
Alisema baada ya Kuwanyan’ganya silaa hizo watu hao
walikimbia kwa kutumia gari ambalo walishindwa kutambua namba zake kwa urahisi
kutokana na mwendo kasi wa gari hilo.
Aliendelea kusema kuwa, Kuhusu mwanzo wao kuishi katika kijiji hicho, kulikuwa na
Pori ambalo halijawahi kufanyiwa kazi tangu mwaka 1982 na ndipo wanakijiji wakaamua Kufyeka na kufanya makazi kwani
wananchi walikuwa wanashida ya mahali pa kuishi.
Gazeti hili lilimtafuta Mzee Cheyo na likazungumza naye a alisema kuwa anasikitika sana kuja nkutishiwa maisha watu
hao kwani yeye anawatoto wanaomtegemea na sasa wakifukuzwa maeneo hayo watakuwa
hawana mahali pa kwenda kuishi hivyo watakuwa kama watoto wa mitaani.
Mzee cheyo aliishauri serikali kuwalinda wananchi wake kwani
wapo wengi wenye shida ya makazi wakati kuna watu waliojilimbikizia mapori
pasipo kuyaendeleza.
Gazeti hili Pia
lilifika Ofisi ya Serikali ya Mtaa ya Mabwepande ambapo ilidaiwa kuwa Bunduki hizo zilifikishwa na kufanikiwa
kumkuta Mlinzi aliyepokea Bunduki hizo na alikiri kuzipokea na kusema kuwa Tayari zimefikishwa katika Kituo
cha Polisi Kawe.
Jitihada za Kumtafuta mkuu waq Kituo cha Kawe hazikufanikiwa
baada ya Simu yake ya Mkononi kutopatikana.