Thursday, August 9, 2012

GARI LA ABIRIA LAWAKA MOTO GHAFLA NA KUTEKETEA

Gari la Abiria maarufu kama Daladala linalofanya Safari zake Kariakoo na Viwandani, limelipuka leo maeneo ya Buguruni Sokoni na kuanza kuteketea kwa moto likiwa safarini kuelekea Viwandani likiwa linatoka Kariakoo.Kwa Mujibu wa Dereva wa Gari hilo ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema kuwa chanzo cha Gari hilo kulipuka ni Hitilafu iliyokuwa katika Gari hilo. MAASINDA ilishuudia  udhaifu wa Gari hilo kwani katika gari hilo hakukuwa na Gesi ya Kuzimia moto(Fire Extinguisher) Hakuna Abiria aliyeumia kwani baada ya kuona Gari linawaka abiria walitoka Nje.

Askari wa Usalama Barbarani nao walikuwepo na wakawa wanapiga picha kwa kutumia simu zao za mkononi

Gari ndo hili na namba zake za usajili ndo hizi

Liliteketea likawa hivi, Na hakukuwa na msaada wowote uliopatikana kuweza kuliokoa gari hilo mpaka maasinda inaondoa mitambo yake hapo iliacha Gari likizidi kuteketea.

Jionee