Raisi wa Chama Cha walimu Tanzania Bw, Gratian Mukoba (Kushoto)
akiongea na waandishi wa habari leo katika makao makuu ya Chama hicho jijini
Dar es Salaam kuhusiana na Tamko lao kwa
serikali kutaka iwarudishie madaraka wakuu wote waliovuliwa nyadhifa zao
kwakuwa ni viongozi wa CWT ndio waliohamasisha mgomo. Vilevile chama kimeitaka
serikali kufuta nia yake ya kuwashitaki
walimu zaidi ya 180,000 walioshiriki mgomo kati ya walimu 233,440 walioko
nchini kwani kwa kufanya hivyo watoto wa maskini wanaotegemea walimu hao
kufundisha watakosa haki yao ya kufundishwa.
Aidha alizungumzia pia baadhi ya wakuu wa mikoa na wilaya kuwaondoa walimu kwenye zoezi la sensa na kusema kuwa
ambapo amesema kuwa wakuu wa
mikoa na wilaya wanafanya hivyo kutokana na agizo kutoka kwa waziri mkuu.
Alisema kuwa, Mikoa iliyo athirika sana
na zoezi hili la kuondolewa katika Sensa ni Dar es Salaam,Pwani,
Morogoro,Iringa, na mikoa mingine, ambapo alisema kuwa walimu watatu wa Shule
ya Sekondari ya Mererani, waliondolewa wakiwa kwenye chumba cha mafunzo kwa
maelezo kuwa walishiriki mgomo.
|