Shirika la umeme Tanzania Tanesco limewatangazia Watanzania wote wanaotumia umeme kinyume na taratibu yaani kwa wizi kujisalimisha ndani ya wiki mbili zijazo kwani Shirika limeanza mkakati wa kupambana na wezi wa umeme ambapo Bi Badra Masoud amesema kuwa yeyote atakayebainika kubypass mita,kuchezea mita, kukata lakiri au seal za mita,amejiunganishia umeme kwa njia isiyo halali atakabiliwa na adhabu zifuatazo, Kutangazwa wazi katika vyombo vya habari, pamoja na kufikishwa katika vyombo vya sheria ikiwemo polisi na hatimaye mahakamani. Badra amesema kuwa Mkurugenzi wa Tanescop ametoa wiki mbili za kujisalimisha kwa wateja wote wenye wasiwasi na matatizo na matatizo ya mita zao. Na ametoa tahadhari kwamba ifikapo mwisho wa mwezi huu wale wote wanaoiba umeme kwa njia yoyote ile wanashauriwa waende wenyewe kwa mameneja wa mikoa na kusisitiza kuwa watakaojisalimisha hawatakuwa na adhabu yoyote zaidi ya kulipa Gharama walizokuwa wanatumia.Aidha wadaiwa sugu pia wametakiwa kulipa madeni yao kabla ya mwezi huu. |