|
Mchezaji wa Timu ya Simba Emmanuel Okwi akipokea Tunzo yake aliyopewa leo katika Tamasha la Simba Day, kama mchezaji bora wa mwaka katika Timu ya Simba. |
Klabu ya Simba leo imefanya
tamasha lao kubwa la kila mwaka maarufu kama Simba Day, kama ilivyokuwa kwenye
miaka mingine iliyopita klabu hiyo leo ilitoa tuzo mbalimbali kwa wachezaji wa
timu hiyo pamoja na watu wengine.
Kwa upande wa wachezaji Marehemu Patrick Mafisango alipewa tuzo ya
heshima, Shomary Kapombe akatwaa tuzo ya mchezaji mwenye nidhamu huku talk of
the town Emmanuel Okwi akichukua tuzo ya mchezaji bora wa klabu hiyo kwa msimu
uliopita.
Watu wengine waliotwaa tuzo ni mwanachama wa siku nyingi wa klabu
hiyo Professa Philemon Sarungi ambaye alipewa tuzo ya kuwa mtu aliyetoa mchango
wa muda mrefu katika klabu hiyo, Haidari Abeid maarufu kama Muchacho aliyetwaa
tuzo ya mchezaji wa bora wa Simba wa miaka ya 70′s, Hamisi Kilomoni – mchezaji
bora wa miaka ya 60′s. Ally Sykes akapata tuzo ya heshima na udhamini.
|
Emanuel Okwi wa pili kutoka kulia akiongozana na wachezaji wenzake kabla ya mchezo wa kirafiki kati yao na Nairobi City Stars ambapo Simba ilichapwa 3-1 |
|
Hichi ndio kikosi cha Nairobi City |
|
Simba A.K.A Wanyama |
|
Mchezaji wa timu ya Simba akimiliki mpira mbele ya beki wa
timu ya Nairobi City Stars katika mchezo wa kirafiki wa tamasha la Simba Day
linalofanyika kwenye uwanja wa Taifa Tamasha hilo limeandaliwa na klabu ya
Simba na hufanyika kila mwaka Agosti 8 na kushirikisha timu marafiki wa
klabu hiyo huku wachezaji na viongozi mbalimbali wakipewa zawadi kwa mchango
wao kwa klabu hiyo, Katika mchezo wa leo, hivi sasa mpira umekwisha na Simba
imefungwa magoli 3-1 na timu ya Nairobi City Stars kutoka nchini Kenya
|