Wednesday, August 8, 2012

GARI LA NAIBU WAZIRI WA AFRIKA MASHARIKI LILIVYOPINDUKA


Naibu waziri wa Afrika Mashariki Abdullah Juma Saddallah amepata ajali ya gari alilokua akisafiria kwenye eneo la Kongowe Kibaha mkoani  Pwani  jana wakati akitokea Dodoma kuja Dar es salaam.
Ajali imetokea leo jioni ambapo Naibu waziri amesema hali yake sio mbaya sana ila dereva ndio ameumia kiasi, bado wanapata matibabu kwenye hospitali ya Tumbi Kibaha Pwani,  chanzo cha ajali amesema ni baada ya dereva wake kukwepa lori lakini hakufanikiwa na gari ikatoka nje ya barabara.