Sunday, August 12, 2012

RAIS KIKWETE AONANA NA RAS MPYA WA GHANA ASHUHUDIA KILIMO CHA MANANASI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Rais John Dramani Mahama wa Ghana nyumbani kwake jijini  Accra leo Agosti 11, 2012 baada ya  kumtembelea na  kumpa pole ya msiba wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Marehemu John Evans Atta Mills aliyezikwa jana.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitazama ukulima wa kisasa wa manasi yanayolimwa  kwa ajili ya kuuzwa nje ya nchi katika shmaba la   Bomarts Farms Ltd. katika kijiji cha Dobrokatika eneo la Nsawam  nje kidogo ya jiji la Accra leo Agosti 11, 2012. Kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa shamba hilo Bw. Anthony Botchway na mwenye suti ya buluu ni Waziri wa Chakula na Kilimo Mhe Kwesi Ahwol

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitazama manasi yakitayarishwa kwa ajili ya kusafirishwa na kuuzwa nje ya nchi katika kiwanda cha  Bomarts Farms Ltd. katika kitongoji cha Dobro nje kidogo ya jiji la Accra leo Agosti 11, 2012.
PICHA NA IKULU