Sunday, August 12, 2012

DK ULIMBOKA AREJEA NCHINI AKIWA FITI

Kiongozi wa jumuiya ya madaktari nchini Tanzania, Dk. Steven Ulimboka, akiwa amebeba maua, na kuzungukwa na Madaktari wenzake na wananchi wa kawaida waliofika kumlaki, mara alipowasili mapema leo Agosti 12, 2012, kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akitokea kwenye matibabu nchini Afrika Kusini. Dk Ulimboka alisema kuwa yuko fiti na anaweza kufanya shughuli zozote atakazopewa kuanzia sasa.