Huyu ndiye mtoto aliyeokotwa katika eneo la PPF Tower jijini Dar es Salaam
saa sita mchana wa leo. Amekutwa amelala chini eneo hilo.
Alipelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na Askari wa Central Police. Mtoto
huyu anakadiriwa kuwa na umri wa mwaka mmoja na nusu hivi, kwa hiyo
hawezi kuongea.
Yeyote anayemfahamu mtoto huyu au wazazi wa mtoto huyu ajitokeze na
kutoa taarifa sahihi kwetu kupitia namba yangu 0755 64 86 36 au 0715 64
86 36.
Mtoto tunaye Hospitalini, anaendelea kuhudumiwa. Tafadhali sambaza barua pepe hii.
Imetolewa na;
Aminiel Buberwa Aligaesha
Afisa Uhusiano Mwandamizi, Hosipitali ya Taifa Muhimbili |
|