Saturday, August 4, 2012

MSANII ROMA ANUSURIKA KUFA BAADA YA AJALI ILYOHUSISHA GARI LAKEALI LEO JIJINI DAR ES SALAAM

Roma akisikitikia Gari lake mara baada ya kupata  ajali leo hii katika Barabara ya Morogoro Road jijini Dar es Salaam
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya anayeimba Hip Hop Roma Mkatoliki amepata ajali mbaya ya gari katika Barbara ya  Morogoro.

Kwa mujibu wa djchoka.blogspot.com ni kwamba tairi la mbele lilipopasuka na gari likaacha njia na kugongana uso kwa uso na fuso ambalo lilikuwa upande wa pili na gari hilo dogo alilokuwa akiendesha Roma kurudi lilipotokea.
Roma amemuambia Dj Choka kwamba anaelekea hospital kwa check up zaidi ila aliokuwa nao kwenye gari hakuna aliyeumia.

Roma amepata ajali hii leo ikiwa ni siku 18 tu toka msanii mwingine wa bongofleva Chege kupata ajali ya gari yake kwa kumgonga mtu wa pikipiki alieingia barabarani ghafla na kusababisha gari kuharibika.

Gari ni nyang'anyang'a