Mserbia Milovan Cirkovick amerejea
usiku wa kuamkia leo kutoka kwao Serbia, alipokuwa kwa mapumziko mafupi, baada
ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, ambayo
timu yake ilitolewa katika hatua ya Robo Fainali kwa kufungwa 3-1 na Azam FC.
Milovan anatarajiwa kuendelea sasa
na kazi ya kukiandaa kikosi chake kwa ajili ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara, inayoanza mwishoni mwa mwezi huu, akianza na mechi ya Ngao ya Jamii,
dhidi ya Azam FC.
Wakati Milovan akitua jana,
mahudhurio ya mazoezi ya Simba ambayo pia itashiriki Kombe la Banc ABC Super 8,
michuano inayoanza kesho, bado si mazuri.
Ni wachezaji 16 tu waliohudhuria
mazoezi ya asubuhi ya leo, ufukwe wa Cocoa Beach, Oysterbay, Dar es Salaam,
wakiwemo wawili wapya, Mrisho Khalfan Ngassa kutoka Azam FC na Cassian Ponella
kutoka Kagera Sugar.
Waliofanya mazaoezi leo ni Juma Kaseja, Hamadi
Waziri, Shomary Kapombe, Nassor Masoud ‘Chollo’, Amir Maftah, Paul Ngalema,
Juma Nyosso, Cassian Ponella, Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto, Kanu Mbivayanga,
Mrisho Ngassa, Haruna Moshi, Haruna Shamte, Kiggi Makassy na Salim Kinje | |