MKUU wa Wilaya (DC) ya Geita, Manzie Omari, ametangaza kupambana kufa na
kupona na mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima, Victor
Eliud, kwa madai ya kumchafua.
Pia,
amemtishia maisha mwandishi huyo akisema atakiona cha moto ikiwa ni
pamoja na kumfikisha mahakamani kama hatakoma kile alichokiita kuandikwa
vibaya katika baadhi ya tuhuma zinazomkabili.
Mkuu
huyo wa wilaya alitoa kauli hiyo siku chache baada ya gazeti la
Tanzania Daima kuchapisha habari iliyokuwa na kichwa kisemacho “CUF
wamshitaki DC kwa RC”, ikinukuu barua ya chama hicho kwenda kwa RC
Magalula kuelezea namna ya utawala wa mkuu huyo wa wilaya ulivyo wa
kibabaishaji, hivyo yeye kusema ililenga kumchafua.
Katika
mazungumzo ya njia ya simu Agosti 23 mwaka huu, yaliyodumu kwa zaidi ya
dakika 20, mkuu huyo wa wilaya hakutaka kumpa nafasi ya kuzungumza
mwandishi huyo isipokuwa kumshambulia moja kwa moja.
“Hivi
wewe Victor unanitafuta nini? Unadiriki kutumia kalamu yako kunichafua
siyo? Unatumiwa na huyo kiongozi wa CUF kunichafua mimi. Nataka
kukueleza nimekuwa DC kwa muda mrefu wala sikuanzia hapa (Geita).
Mwambie huyo Malugu kwamba ofisi yangu haina muda wa kujibu barua
zake.... “Na kama huyo Malugu ana ndoto za kuwa DC, mwambie hataupata hadi anaingia kaburini. Hakuna rais wa kumteua akae akijua,” alisema.
Mbali
ya hayo, DC huyo alimweleza mwandishi huyo kuwa kuanzia sasa, ni adui
yake na kwamba hataki kushirikiana naye kwa namna yoyote ile. SOURCE WAVUTI-WAVUTI
