|
Raisi wa Chama cha walimu CWT Gratian Mukoba (kushoto)
wakijadiliana jambo na Mkuu wa Idara ya
Elimu na Mafunzo Bw, Anthony Mtavungu.
|
Chama cha walimu nchini Tanzania kimetoa wito kwa serikali
kuacha kupuuza amri ya mahakama ikiwa ni pamoja na kuwahurumia walimu kwani walimu wanamaisha magumu hivyo
wanahitaji kusikilizwa na muajiri wao ili wapate mishahara inayokidhi mahitaji
yao.
Akizungumza na waandishi wa habari leo katika makao makuu ya
Chama hicho jijini Dar es Salaam Rais wa Chama hicho Bw, Gratian Mukoba amesema kuwa Kitendo cha serikali kukaa kimya
kwa muda wa siku 27 bila ya kuonyesha kujali kutekelezwa kwa amri ya mahakama
iliyokuwa inaitaka serikali kufanya mazungumzo na walimu chini ya mshauri
mtaalamu wa sheria za kazi ni dhahiri kwamba, serikali haoina nia njema ya kusikiliza madai ya walimu.
Bw Mukoba amesema kuwa, tayari wameiandikia barua serikali
lakini mpaka sasa hamna jibu lolote wala nia iliyoonyeshwa na serikali ya
kutaka kukaa mezani kufanya majadiliano kama walivyoagizwa na mahakama.
Kufuatia malalamiko ya CWT chama hicho kimeitaka
serikali kuhakikisha kuwa mazungumzo
kati yao na Serikali kuwa yanaanza kusikilizwa kabla ya shule
kufunguliwa tarehe 10 september 2012 na pia Serikali ihakikishe kuwa walimu
wote waliovuliwa madaraka kwa kisingizio kuwa wameshiriki mgomo wanarudishiwa
vyeo vyao vinginevyo chama kitaamini kuwa
walimu wanapewa madaraka sio kwa uwezo wao bali kwa unyenyekevu uliovuka
mipaka.
| Baada ya mazungumzo na waandishi wa habari |