Thursday, August 30, 2012

BI HAWA NGULUME AFARIKI DUNIA

Taarifa tulizozipata hivi punde ni kuwa aliyewahi kuwa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Bagamoyo na Mbarali kwa vipindi tofauti na kushika nyadhifa mbalimbali katika Chama Cha Mapinduzi, CCM, Bi. Hawa Ngulume amefariki dunia katika hospitali ya Jeshi ya Lugalo, jijini Dar es Salaam leo asubuhi.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana amesema taratibu za mazishi zinaandaliwa na taarifa kamili itatolewa baadaye.


Mama Ngulume amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya saratani kwa kipindi kirefu ambayo ndiyo yaliyompelekea kifo chake.


Pole kwa wote mlioguswa na msiba huu.

Roho ya marehemu ipumzika pema.
AMIN.