Mstahiki
Meya wa manispaa ya Ilala Jerry Silaa alipokuwa akimkabithi katibu wa UVCCM mkoani Mwanza Bw Elias Mpanda, fomu alizorejesha jana za kugombea
nafasi ya ujumbe wa UVCCM-NEC
jana katika ofisi za CCM mkoa- Jijini Mwanza. Mstahiki meya Manispaa ya Ilala
Bw Jerry Silaa anagombea nafasi ya ujumbe wa UVCCM-NEC ngazi ya taifa.Mstahiki
meya aliweka wazi nia yake ya kutaka kuwawakilisha vema vijana wa
kitanzania kwenye UVCCM-NEC na aliwaasa vijana wengine kushiriki kwenye
mchakato huo na huku akisisitza kwamba yuko tayari kufanya kazi kokote nchini
kwa maslahi ya wananchi, vilevile meya aliwaasa viongozi wote kuwajibika na
kutimiza ahadi zao walizozitoa kwa wananchi na kwa kuweka mbele maslai ya
taifa na sio yao binafsi.
|