Mwigulu
Nchemba , juzi jumatatu amechapisha tisheti zenye maandishi ya M4C – na ameweka
maana kwenye hizo tisheti ambazo bado hazijaanza kugawanywa kuwa ni Movement 4
Chagga na ameweka maandishi makubwa kuwa changia Movement 4 Chagga (M4C), Zipo
na zitaanza kugawanywa muda wowote .
Zoezi
hili linaendena sambamba na operation ya Mwigulu ya kwenda Igunga eti kuelezea
nini kilitokea mahakamani kwa wana Igunga , ziara hii imepangwa kuanza siku ya
Jumamosi kwani alikuwa anasubiria FUSSO waliyonunua kwa shilingi milioni
arobaini na tisa (49,000,000) na kuitengeneza kama za CDM ikamilike na
walinunua vifaa Mlimani City tayari tangu wiki iliyopita.
Lengo
la kuweka hapa ni kuwajulisha CDM wajue kuwa kuna mipango hiyo tayari imepangwa
na inaendelea kutekelezwa , chukueni hatua .Aidha kuna vijana wenu watatu
majina leo nayahifadhi wanafanya vikao vingi sana na Mwigulu na wa mwisho
alipofika kwake wiki iliyopita alipewa shilingi laki nane , mara ya kwanza
alipewa shilingi milioni tatu na huyu ametangaza rasmi kuwa atajiunga na CCM
wakati wowote – fuatilieni waliogombea Bavicha na kushindwa na hata mmoja
aliweza kushinda ila anawahujumu nyie CDM.
source: Jamii forum
|