1.Amini nawaambieni enyi Waswahili wachache mnaotawala; mnategemea kweli kuwa
mtawaongoza Watanzania kwa lazima wakati wamepoteza matumaini, na mtegemee kuwa
watasalia wamekaa kimya kwa amani na utulivu?
2.Amani ni zao la matumaini, pindi matumaini yatakapotoweka kutakuwa na vurugu
katika jamii.
3.Nitashangaa kama hawa Watanzania watakataa kuasi. Kwanini wasiasi?
4.Wakati wengi wa wananchi wanapopoteza matumaini
unajenga volcano. Volcano hii italipuka siku moja. Labda kama watu hawa ni
wajinga.
5.Na hakutakuwa na watu wa kizazi hiki na karne hii ambao watatakiwa kujitoa
muhanga kwa ajili ya maisha bora katika siku zijazo wakakubali, wakati
wanawaona watu wachache wakiendelea kuneemeka machoni pao bila kujali wakati
ujao, wakati wao na watoto wao wakiendelea kuishi katika maisha duni na
dhalili.
6.Watanzania watakuwa ni wajinga na mataahira, kama watakubali kuendelea
kukandamizwa na watu wachache katika nchi yao