Rais wa Chama Cha walimu Tanzania Bw, Gratian Mukoba
akiongea na waandishi wa habari leo katika makao makuu ya Chama hicho yaliyopo
Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Baada ya Mahakama kuaamua
kuwa Mgomo wa walimu ni Batili, Chama cha walimu Tanzania CWT kimewataka
walimu kurudi kazini na kuwaomba wawe na uvumilivu kwani chama kitazungumza na
wakili wake ili wakate rufaa.
Rais wa CWT alisema kuwa, Uamuzi wa mahakama kusema kuwa
Mgomo wa walimu ni Batili,Rais alisema kuwa ni Ukatishwaji wa tama kwa walimu
kwani walimu wanataka haki zao. Hivyo akasema kuwa walimu wanarudi Kazini huku
wakiwa wamekata tama.
|