Baraza la
Vijana la Chadema (BAVICHA) limetoa tamko lao leo jijini Dar es Slaam kuhusiana
na Maamuzi ya Serikali juu ya Mgomo wa Walimu.
Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari Katibu mkuu wa BAVICHA Bw, Deogratias Siale alisema kuwa wao kama Bavicha wanaitaka
serikali kushughulikia mara moja Madai ya walimu haraka na kwa busara ili kurudisha ari ya walimu itakayofanya
waweze kufundisha ipasavyo.Alisema kuwa sio halali serikali kusema kuwa haiwezi
kutimiza madai ya walimu kwa asilimia
miamoja wakati inatumia kiasi cha
shilingi bilioni 900 kulipa posho watumishi wa Umma wakiwemo watendaji wa
serikali na wanasiasa kwenye posho za kukaa.
Bw, Siale
amezungumzia pia Swala la Dk Ulimboka na
kusema kuwa serikali iachane na Filamu
kwa kujisafisha kwa kashfa ya kumteka na
kumteka Dk Ulimboka. Alisema kuwa
shahidi mzuri anayeweza kusema ukweli kuw a serikali inahusika au la ni Dk
Ulimboka mwenyewe kwani naye anayo fursa ya kuweka mambo haya bayana.
Pia
alizungumzia tuhuma za Rushwa Bungeni ,na kusema kuwa wanamtaka Spika wa Bunge kuacha kuchunguza wale wanaotuhumiwa kupokea
rushwa peke yao kutoka Tanesco bali pia awashughulikie na wale waliotajwa
kuomba rushwa kutoka kwa wakurugenzi wa
halmashauri
|