Thursday, August 2, 2012

RAIS KIKWETE AGAWA NG'OMBE 1500 MKOANI ARUSHA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na viongozi wengine wa serikali akiwemo William Lukuvi,.Rais Kikwete jana amefika katika kijiji cha Makuyuni wilayani Monduli, kuzindua mpango wa kugawa ng'ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha (Longido,Monduli na Ngorongoro) kama kifuta jasho cha kupoteza mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake zilizotokea mwaka 2008/2009.

Hapa akisalimiana na  Mbunge wa Monduli Edward Lowasa

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Baadhi ya Viongozi wa Serikali wa Mkoa wa Arusha waliofika katika kijiji cha Makuyuni,Wilayani Monduli kumlaki.Rais Kikwete leo amefika katika kijiji hicho cha Makuyuni na kuzindua mpango wa kugawa ng'ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha (Longido,Monduli na Ngorongoro) kama kifuta jasho cha kupoteza mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake zilizotokea mwaka 2008/2009.

Hawa ndio baadhi ya Mifugo hiyo