Sunday, August 5, 2012

CUF WALAANI MAJIBU YA SERIKALI KWA WALIMU

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi Cuf Profesa Ibrahim Lipumba, akiongea na waandishi wa Habari leo katika makao makuu ya Chama hicho jijini Dar es Salaam juu ya Kusikitika kwao kwa majibu ya Serikali kutokana na madai ya walimu.
 Ili walimu waweze kufundisa kwa weledi na wanafunzi waweze kuelewa ipasavyo, serikali imeshauriwa kushugulikia madai ya walimu kwa asilimia zote kwani inayo uwezo endapo ikitilia maanani swala hilo.
Hayo  yamesemwa hii leo, na Mwenyekiti wa Chama cha wananchi Cuf Prophesa Ibrahim Lipumba wakati akiongea na waandishi wa habari katika makao makuu ya Chama hicho jijini Dar es Salaam.
Prof Lipumba alisema kuwa, Endapo itapunguza matumizi katika sekta mbalimbali za umma kama Magari ya Kifahari ya viongozi wa serikali, Posho na mengine yote yanayofanana na hayo yasiyo ya Lazima  Serikali itaweza kutatua tatizo la walimu kwa asilimia zote wanazozitaka walimu.
Aliongeza kuwa Srerikali haiwezi kusema kuwa hawana pesa ya kuwalipa walimu wakati walimu wenyewe wanajua Posho za wabunge, wakurugenzi wa wizara pamoja na wakurugenzi kwa hivyo kama hizo Posho zikipunguzwa tatizo la walimu litatatuka kwa urahisi.
Aidha Lipumba alisema kuwa Serikali inapaswa kushughulikia wananchi wake na sio mpaka wasubiri mgomo kwani Mgomo unapotokea kuna wananchi wengine wanaoathirika kutokana na Mgomo huo.
“Serikali inapaswa kushughulikia matatizo ya wananchi mapema ili kuepusha migomo inayojitokeza mara kwa mara”amesema Lipumba. 
Waandishi wa Habari wakimsikiliza Lipumba kwa Makini

Hapa wapo kazini