Siku chache baada ya
kushindwa kutwaa ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati maarufu kama Kombe la
Kagame klabu ya soka ya Azam Fc imemtimua kocha wake mkuu Muingereza Stewart
Halll, imefahamika.
Habari kutoka ndani
ya klabu hiyo zinaeleza kwamba sababu ya kumtimua kocha huyo ni kitendo cha
kumpanga nyota wa timu hiyo Mrisho Ngassa katika mechi ya fainali ya Kombe la
Kagame baina ya Azam na Yanga ambapo Yanga ilitwaa ubingwa baada ya
kuifunga Azam mabao 2-0.
Inaelezwa kuwa
uongozi ulikerwa na kitendo cha Ngassa ambaye kwa muda mrefu amekuwa
akituhumiwa kuwa na ‘Uyanga’ na hivyo kocha kumuweka benchi katika mechi za
kombe la Kagame, alipoibusu na kuvaa jezi ya Yanga baada ya mchezo baina ya
Azam na Vita.