Club ya Real Madrid imetangaza kwamba Mchezaji
Legend wa soka wa Ufaransa Zinadine Zidane atakua kocha wa moja kati ya timu za
vijana za Real Madrid.
Zidane mwenye umri wa miaka 40 ambae alistaafu
kucheza soka miaka sita iliyopita baada ya kumpiga kichwa mchezaji Marco
Materazzi kwenye fainali ya kombe la dunia ishu ambayo ilimfanya aape kwamba
hatorudi tena uwanjani, anataka kurudi kwenye soka lakini akiwa kama kocha.
Mpaka sasa amezichezea club kama Cannes, Bordeaux,
Real Madrid na Juventus ambako kote huko alifanikiwa kuzigonga nyavu mara 95
toka ameanza kucheza soka mwaka 1988.
Zinedine Zidane atakua anaendelea na masomo yake ya
ukocha wakati akiifundisha timu hiyo ya vijana na anatarajia kumaliza hiyo kozi
ya ukocha mwaka huu.
Zidane anatarajiwa kuchukua nafasi ya Alberto
Giraldez kama mkuu wa timu za vijana wa Real ingawa club hiyo haijathibitisha
hizo stori mpaka sasa.
Zidane ambae ameshinda mara tatu kuwa mchezaji wa
dunia wa Fifa amewahi kusema kwamba ana ndoto za kuwa mwalimu wa soka siku moja
na pia kuifundisha timu ya taifa ya Ufaransa.
|