Monday, June 22, 2015

JINSI MAJAMBAZI WALIVYOJARIBU KUPORA FEDHA KWENYE GARI NA KUKAMATWA WAWILI

Gari lililoporwa likiwa na matundu ya risasi.
Polisi wakiwa eneo la tukio.
Mmiliki wa gari kushoto akitoa maelezo kwa polisi. (DK)
Askari wa usalama barabarani akilikagua gari.
MAJAMBAZI wanaokadiriwa kuwa watatu leo mchana wamefanya uporaji kwenye maduka matatu ya kutoa na kuweka fedha kwa njia ya simu maeneo ya Mikocheni Kwa-Mwalimu Nyerere jijini Dar ambapo baadaye walitoroka na wawili kati yao kukamatwa.
Mashahidi waliokuwepo aneo husika walisema baada ya uporaji huo, majambazi hao  walipora gari aina ya Suzuki-Vitara na kuondoka nalo lakini walipofika mita chache karibu na baa maarufu ya Rose Garden, gari hilo liliwagomea kwenda na kuanza kupiga king’ora cha hatari (alarm) kitendo kilichowafanya washuke na kuanza kutafuta njia nyingine ya kujiokoa ambapo aliyeshika ‘fuba’ la fedha alifanikiwa kupora pikipiki aina ya Boxer na kutokomea na wawili waliokuwa wakitafuta njia ya kujinasua walitiwa mbaroni na askari polisi waliokuwa wakiwafukuza.
(GPL) 

No comments:

Post a Comment