Tuesday, December 2, 2014

DIAMOND PLATNUMZ ALIVYOFANYA KWELI TUZO ZA CHANNEL O NCHINI AFRIKA KUSINI

Mrembo Zari anayedaiwa kuchukua nafasi ya Wema Sepetu akiwa ameshika tuzo za Diamond.
Diamond Platnumz akipozi baada ya kutwaa tuzo tatu za Channel O jana usiku nchini Afrika Kusini.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Diamond Platnumz akiongea machache baada ya ushindi huo wa kishindo.
Diamond katika pozi na wadau.
Diamond katika pozi na wadau pamoja na mama yake mzazi, Sandra (wa pili kulia).
Diamond (katikati) akiwa na management yake. Kulia ni Said Fella na Babu Tale (kushoto).
Mama mzaa chema, Sanura 'Sandra' Kassim katika pozi.
Kutoka kushoto ni Mama mzazi wa Diamond 'Sandra', Diamond na Zari katika picha ya pamoja.
MSANII Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ ametwaa tuzo tatu za Channel O jana usiku nchini Afrika Kusini. Tuzo hizo ni; Most Gifted new comer, Most Gifted Afropop na Most Gifted East kupitia wimbo wake wa Number One.
Kupitia ukirasa wake wa Facebook Diamond amewashukuru sana mashabiki wa wote walio msupport.
"Kiu kweli, haikuwa rahisi kabisa.. lakini kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na support kubwa mliyonipa iliwezesha Bongo Flavour yetu kuandika historia mpya kwenye ramani ya muziki wa Afrika...Hii inaonyesha ni jinsi gani umoja ni nguvu na pia jinsi gani muziki wetu ukisupportiwa na kupewa kipaumbele unaweza kufika mbali zaidi... Shukrani sana kwa @channeloafrica @channelotv kwa kuniona na kuthamini kipaji changu, My Family, Management, Media zote zilizokuwa zikinisupport, Watangazaji, Wasanii, Wadau na bila kuwasahau wapendwa wangu" - Ameandika Diamond.GPL

No comments:

Post a Comment