Watoto wawili wa kiume wenye umri wa miaka 11 na 13 wameshushiwa makonde wanafunzi wenzao na kuwaita jina la ‘Ebola’.
Watoto hao wawili raia wa Senegal
walihamia Marekani mwezi mmoja uliopita ‘waliporomoshewa kipigo’ wakiwa
shuleni I.S 318, New York katika viwanja vya michezo ambapo wenzao
waligoma kushiriki nao michezo na kwa kile walichodai wataambukizwa
Ebola na baadaye kuwazonga na kuwapiga.
Taarifa zinasema baba wa watoto hao,
Ousame Drame amekuwa akipewa taarifa na watoto wake kuwa tangu wafike
shuleni hapo wamekuwa wakinyanyapaliwa kwa kuitwa Ebola, kitu ambacho
kimekuwa kikiwakasirisha na kumtaka baba yao awarudishe Senegal.
Idara ya Elimu New York imethibitisha kupokea taarifa zinazohusu vijana hao.
Baba huyo amesema japo watoto hao
wamekulia Senegal lakini wana haki za kuishi Marekani kwa kuwa
walizaliwa huko, na moja ya matatizo linalowakabili ni kutokujua lugha
ya kiingereza kutokana na kukulia nchini Senegal ambako inazungumzwa
lugha ya Kifaransa.
No comments:
Post a Comment