Thursday, October 9, 2014

WALE ASKARI WALIOKUWA WANAFANYA UFUSKA NA SARE ZA POLISI HATIMAYE WAMEFUKUZWA KAZI, NI PAMOJA NA ALIYEWAPIGA PICHA


askari 2Kama kila siku huwa unaingia facebook, whatsapp au instagram inawezekana ukawa ulikutana na hii picha ya Askari Polisi ambao walipigwa picha wakiwa wanakiss wakiwa ndani ya sare za jeshi hilo.
Sasa taarifa mpya iliyotoka baada ya hii picha kuzidi kusambaa ni kwamba Jeshi la Polisi Kagera limechukua maamuzi ya kuwafukuza kazi askari hawa wawili pamoja na mwingine mmoja ambae ndio aliipiga hii picha kupitia simu yake ya mkononi.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Henry Mwaibambe amewataja askari hao kuwa ni PC Asuma Mpaji Mwasumbi mwenye namba F.7788,PC Fadhili Linga mwenye namba G 2122 na PC Veronica Nazaremo Mdeme na wote walikuwa askari wa kikosi cha usalama barabarani wilayani Missenyi.
ASKARIKamanda Mwaibambe amezungumza na ITV na kusema askari hao walitenda kosa hilo la fedhea kwa kupiga picha kinyume na maadili ya jeshi hilo mwaka 2012 wakiwa kazini na kwamba PC Fadhili ndiye aliyehusika na kupiga picha hizo kwa kutumia simu yake ya mkononi na kuituma katika mitandao mbalimbali ya kijamii kitendo ambacho ni kinyume cha maadili kwa sababu mbalimbali.
Mwaibambe amekiri kuwa picha husika inayoonekana kwenye mitandao ni picha halisi ambayo haijachakachuliwa hivyo ni wazi kila askari kujua maadili ya kijeshi yapo kisheria na askari yeyote anafundishwa namna ya kuishi katika maisha ya utumishi wa jeshi la Polisi.

No comments:

Post a Comment