Raia wa Tanzania anayeishi katika jiji la Melbourne, Australia,
Charles Amon Mihayo, 36, aliwanunulia binti zake Savannah, 4, na
Indianna, 3, gauni za dance ya ballerina, akawaangalia wakidansi, kisha
akawaua wote wawili.
Baada ya kuwaua mabinti hao, Mihayo aliwapigia simu polisi
kuwataarifu, kisha aliiogesha miili ya marehemu, na wakati akiivalisha
nguo miili hiyo, aliwaambia polisi waliofika na kugonga mlango, wasubiri
kidogo.
Alipofungua mlango, polisi walimuuliza, kwanini amewaua watoto wake.
Mihayo alijibu kuwa hakuna “good reason for what he did but it made
sense to him at the time” [hakuwa na sababu ya maana ya kuwaua, lakini
aliona ni kitu cha busara wakati anafanya mauaji hayo.]
Mtuhumiwa alisema kuwa hakupanga kuwaua binti zake, lakini hiyo
haijalishi sasa maana maji yameshamwakiga; na kwamba hakutakiwa kufanya
vitendo hivyo lakini ndio imeshatokea.
Dakika tisa baada ya Mihayo mwenyewe kuwapigia simu polisi na
kuripoti kuwaua wanae, mama wa watoto hao aliwapigia simu ya dharura
polisi kuwataarifu kuwa kuna kitu kimewatokea wanae waliokuwa wameenda
kumtembelea baba yao.
Ripoti ya polisi inasema siku moja kabla ya tukio, Mihayo alimtumia
text-message mama wa wanae, ambaye ndiye aliyekuwa akiishi na watoto
hao, kumuomba awapeleke watoto wakamtembelee ili awaone mara ya mwisho.
Siku hiyo, kabla ya kutembelewa na wanae, Mihayo aliwanunulia watoto
hao gauni na viatu. Mama na watoto walipofika nyumbani kwa Mihayo,
apartment ambayo amepangisha kutoka kwa bibi wa wanae, Mihayo alimuuliza
mzazi mwenza ana muda kiasi gani na wanae, kisha akawaingiza watoto hao
ndani ya apartment yake.
Mama na bibi waliwasikia watoto wakicheza, kabla ya mmoja wa watoto
hao kutoka barazani akiwa amevaa gauni ya maua na viatu vyeupe
alivyonunuliwa na baba yao.
Mtoto huyo alianza kudansi kabla ya baba yake kumuita arudi ndani,
ili ajitayarishe kumuonyesha mama kitu kingine dakika kumi baadae.
Baadae kidogo, mama na bibi waliona watoto wamekuwa kimya. Mama
aligonga mlango, Mihayo akamwambia asubiri kidogo. Mama huyo akagonga
tena. Mihayo akafoka “utajua polisi watakapokuja!” Mama alikimbilia
kwenye sebule ya mama yake na kuwapigia simu polisi. Polisi, ambao
tayari walishapigiwa simu na Mihayo mwenyewe, walipogonga mlango, Mihayo
aliwajibu “I’m just finishing up.”
Alipofungua mlango, huku akifuta mikono yake na taulo, aliwaambia
polisi: “tayari nimemaliza…Nimeshawaua” [It's done, I've killed them.]
Mihayo, ambaye alikiri kuwaua watoto hao kwa kuwakaba baadae
aliwaambia polisi kuwa alikuwa amefurahia mama watoto kuwaleta wanae,
ili aseme “goodbye” kwao kwa mara ya mwisho. Mihayo aliwaeleza kuwa
aliwavalisha wanae gauni za ballerina na mabinti wakaanza kudansi.
“Walienda nje kumuonyesha mama yao nguo zao mpya” alisema Mihayo.
Alisema kuwa watoto waliporudi ndani, alirekodi video na simu yake
watoto hao wakidansi nyimbo ya “Let it Go” kutoka kwenye movie “Frozen.”
Mihayo alisema baada ya nyimbo kwisha, watoto hao walianza kucheza
mchezo wa “hide and seek”(unafanana na kombolela.) Hapo ndipo alipoweka
mto nyusoni mwa watoto wote wawili, na kuwabana mpaka walipoacha
kuhangaika na kupumua.
Baada ya watoto hao kupoteza maisha, Mihayo aliwapigia simu polisi,
na kuwapeleka watoto hao bafuni na kuanza kuwaogesha na kuwavalisha
nguo.
Mihayo hakutoa sababu za mauaji hayo zaidi ya kusema wapelelezi
hawawezi kuelewa “what he has been through” na kwamba kutoa sababu ya
mauaji haitabadilisha chochote.
Mihayo anashikiliwa mahabusu, akisubili kutokea mahakama kuu kukabiliana na tuhuma siku za usoni.
No comments:
Post a Comment