Mwandishi wa habari Badi akilia baada ya kushambuliwa na Polisi,huyu ni moja ya waandishi walioshambuliwa
Kuna
taarifa kuwa mwaandishi wa habari wa IPP Media kapigwa na jeshi la
polisi alipokuwa ameenda kuripoti matukio yaliyokuwa yanaendelea baada
ya mwenyekiti wa CHADEMA Mhe, Mbowe alipoenda kuitikia wito wa jeshi
hilo la polisi.
Habari
zinasema kuwa baada ya Mbowe na wanasheria kuingia ndani polisi walianza
kupiga kila aliyekuwa eneo la tukio bila kujali ni nani ndipo
alipojikuta mwandishi huyo akipigwa mpaka kupoteza fahamu...(MC)
Imeelezwa
kuwa waandishi wengi wa habari wameumia vibaya kutokana na kukimbizwa
na mbwa wa polisi huku wengine wakiumwa na mbwa hao.
Waandishi
wa habari wameshindwa kutimiza wajibu wao kwa kuzuiwa na polisi ambao
wameshindwa kutambua uwepo wa waandishi wa habari,Je Uhuru wa vyombo vya
habari uko wapi Tanzania? na kama waandishi wa habari wameanza kuumizwa
mapemaa kabisa kabla hata kampeni za uchaguzi hazijaanza,Sijui uchaguzi
ukifika hali itakuwaje!!
Ikumbukwe
kuwa Mwaka jana mwandishi wa habari Daud Mwangosi aliuawa kikatili kwa
amri ya RPC (Kamuhanda) wa Iringa wa wakati huo ambaye baada ya kutimiza
azima yake hiyo alipandishwa cheo.
Mami ya
watu leo wamejitokeza kumsindikiza Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, baada ya kuhitajiwa
kufika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi nchini, jijini Dar es Salaam
kuhusiana na kauli yake aliyotoa Septemba 14 mwaka huu,juu ya kuitisha
maandamano nchi nzima kupinga kuendelea kwa Bunge Maalum la Katiba.
Kilichofuata
ni polisi kuamuru watu wote waondoke eneo hilo kwa umbali wa mita 200
ambapo walikimbizwa na mbwa wa polisi na kusababisha wengi wao waumie na
kupoteza vitu vyao mbalimbali, hususani wanahabari ambao baadhi yao
waliumia na kupoteza zana zao za kazi.
CHANZO; GPL
No comments:
Post a Comment