Thursday, July 24, 2014

HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA KWENYE KESI YA MBASHA JANA

Mbasha 22KESI ya ubakaji inayomkabili mume wa Flora Mbasha ambae ni mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili Tanzania Emmanuel Mbasha (32), ilitajwa tena July 23 2014 katika mahakama ya wilaya ya Ilala ambapo Mbasha amesomewa tena mashataka yake huku akikubali sentensi mbili tu kati ya nne zilizosomwa.
Akisoma hoja hizo mbele ya hakimu Wilbert Luago, mwendesha mashtaka wa serikali Nasoro Katunga alisema May 23 2014 mtuhumiwa alimbaka binti aitwaye  Yerusalemu Boazi (17) ambae ni mdogo wa Flora na kumlazimisha asimwambie mtu yoyote ambapo wakati akitenda kosa hilo mkewe Flora hakuwepo nyumbani.
Katunga aliendelea kufafanua kuwa May 25 2014 Mbasha alirudia tena kitendo cha ubakaji baada ya kumuomba binti huyo amsindikize kumtafuta mke wake ambae hakuwepo nyumbani ambapo walipofika Tabata peke yao, Mbasha alimbaka tena binti.
Hizo sentensi zote mbili za juu Mbasha amezikana Mahakamani kwa kusema sio kweli.
Hata hivyo iliendelea kuelezwa kwamba tukio hilo la ubakaji liliripotiwa katika kituo cha polisi Tabata ambako Boazi alipewa PF3 kwa ajili ya kupata matibabu ambapo uchunguzi uliofanywa ulionyesha ni kweli binti huyo aliingiliwa kimwili.
Mbasha 25
Mbasha akiwa na baba yake mzazi Mahakamani.
Katika kesi hiyo ambayo Mbasha anatetewa na wakili Mathew Kakamba, Mbasha alikubali sentensi mbili na kuzikataa mbili zilizobaki kwamba alimbaka binti huyo.
Alichokubali ni kusema ni kweli alimuomba binti huyo amsindikize kumtafuta mke wake ambaye hakuwepo nyumbani na pia alikubali ni kweli Mei 23 2014 mke wake Flora Mbasha hakuwepo nyumbani.
Baada ya kusomewa mashataka hayo na mwendesha mashataka wa serikali, Jaji Luago aliahirisha kesi hiyo hadi August 22 2014 baada ya wakili anayemtetea Mbasha kudai atakuwa na safari kwa siku za karibuni nje ya Mkoa.

No comments:

Post a Comment