Monday, June 2, 2014

ULEVI UTAUA KIPAJI CHA FID Q ONA ALICHOKIFANYA JANAAnaitwa Fid Q mzee wa Mwanza Mwanza anakubalika sana kwa kua mkali wa mashairi yenye vina na yanayofanya mtu afikirie sana ili kuja kumwelewa. Yupo kwenye gemu toka kitambo nakumbuka mimi nlikua shule ya msing wakati naanza kumsikia.

Baada ya ukame wa tuzo hatimaye mwaka huu alichukua tuzo ya mwana HipHop bora katika tuzo za KTMA na akafanikiwa kua moja kati ya wasanii wachache walioshinda tuzo mwaka huu kuchaguliwa kujiunga na Kill Tour ambayo itazunguka miko mbalimbali hapa Bongo.

Jumamosi iliyoisha ilikua zamu ya wakazi wa Mwanza kupata shangwe za Kill Tour na baadhi ya wasanii waliodondosha show ya nguvu ni Vanessa Mdee, Weusi, Ben Pol na Fid mwenyewe. Wasanii wengine wote walipiga show vizuri tatizo lilikuja pale alipopanda Fid jukwaani.

Burudani aliyotoa sio ile wakazi wa Mwanza waliyotarajia inadaiwa kua Fid Q alikua amelewa sana. Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichokua backstage kiliiambia Bongoclan kua kulikua na bia za bure zilizokua zikitolewa kwa wasanii na kampuni ya bia ya Kilimanjaro ndizo zilidaiwa kua chanzo cha Fid kuharibu stejini.

Chanzo hicho kiliendelea kusema kua pamoja na kutoa burudani mbaya lakini alikua akiyumba yumba na kutaka kudondoka. Mwisho wa siku alishuka lakini watu walibaki wakilalamika. Mashabiki wake hawakuridhika wakamfata Insta na kulalamika na haya ni baadhi ya maoni Bongoclan iliyoyapata

salumusaid broo mi nakukubal san ila jan sijafurahia shoo ata kidogo
erickhenry773 Ukaamua kuwa ahmada jana underperfomance kichz

Baada ya kuona watu wamemind sana Fid Q aliamua kufunguka na kusema haya kuhusu kufanya kwake vibaya ''Afya ilileta mgogoro.. Nxt time kama vp.. Pole kwa usumbufu uliojitokeza ��"

No comments:

Post a Comment