Sunday, June 8, 2014

Neno la kwanza la Diamond Platnumz baada ya kutofanikiwa kuchukua tuzo za MTV MAMA.

MWIGIZAJI wa siku nchini, Said Ngamba maarufu kama Mzee Small, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa Rufaa ya Muhimbili mjini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa kwa matibabu.
Mtoto wa marehemu, Muhiddin amethibitisha taarifa za kifo cha baba yake, ambaye alikuwa anasumbuliwa na shinikizo la damu.
Muhiddin alisema baba yake alizidiwa jana nyumbani kwake, Tabata, Dar es Salaam na kukimbizwa Muhimbili, ambako umauti ulimfika.Mzee Small kushoto akiwa na Bi Chau enzi za uhai wake

Mzee Small jina lilitokana na ufupi wake, ni miongoni mwa waigizaji wa mwanzoni nchini waliokuwa wamebakia ambao walifungua njia kwa wengine wengi wanaotamba kwa sasa.
Alipata umaarufu zaidi wakati alipokuwa akiigiza kama mume wa Chausiku Salum ‘Bi Chau’ kuanzia Redioni hadi kwenye Televisheni.
Kwa kwa miaka miwili sasa, afya ya Mzee Small imekuwa ikisumbua na mara kadhaa alilazwa hospitali na kuruhusiwa baada ya ahueni. Mungu aiweke pema peponi roho ya marehemu. Amin. - See more at: http://www.kengete.com/2014/06/msiba-mzee-small-hatunaye.html#.U5Sj_XbZiuI

CaptureMacho na masikio ya Watanzania wengi kwa siku ya Jumamosi June 07 yote yalielekezwa Durban Afrika Kusini sehemu ambako zilikua zikitolewa tuzo za wateule wa MTV Afrika Music Award ‘MAMA’.

Furaha tuliyokuwa nayo Watanzania ilikua kubwa baada ya kuona kijana kutoka nyumbani Tanzania kuwa ni miongoni mwa vijana wanaochuana kwenye tuzo hizo tena akiwa vipengele viwili,ingawa bahati haikua njema kwa Diamond kwani hakufanikiwa kupata.
MOND22Baada ya kutangazwa washindi hao na yeye kutokuwepo Dimaond Platnumz ameandika maneno haya kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii>’Maisha ni Hatua.. Nafkiri kwa mwaka huu ile ndio ilikuwa hatua yetu kwa MTV…Cha muhimu ni kujua wapi tulipokua mwaka jana na wapi tulipo leo… pia kujifunza na kujua ni nini cha kuongeza zaidi ili Next tym tuzidi kufanya vyema…. Shukrani zangu nyingi ziende kwa Mashabiki wote,Management, Media,Family, wasanii na wadau Mbalimbali kwani kwa nguvu zao ndio zimefanya leo kunisogeza toka sehem moja kwenda nyingine…Next stop #BET!!!… Asante sana #Sheriangoi kwa Suti Hii’.
Diamond Platnumz alikuwa pia ni moja kati ya watumbuizaji wa ugawaji wa tuzo hizi,ambapo kwa namna alivyoingia kwenye jukwaa na Davido  ilimfurahisha kila mtu aliyekuepo ukumbini na watu waliokuwa wakiangalia nyumbani kupitia DSTV.

No comments:

Post a Comment