Tuesday, June 10, 2014

MWENYEKITI WA BARAZA LA MAIMAM AUWAWA KWA KUPIGWA RISASI LEO HIIMwenyekiti wa baraza la maimam na muhubiri maarufu nchini Kenya Sheikh Mohammed Idris, ameuawa kwa kupigwa risasi mjini Mombasa.

Sheikh Mohammed Idris ameuawa karibu na msikiti ulio karibu na nyumbani kwake eneo la Likon baada ya kuvamiwa na kundi la watu waliokuwa na silaha, wakati akitoka nyumbani kuelekea msikitini.

Taarifa kutoka katika eneo hilo zinasema kuwa Sheikh Mohammed Idris alikuwa akipata vitisho vya mara kwa mara kutoka kwa kundi la vijana wa kiisilamu wanaodai mabadiliko, na amewahi kutoa taarifa za vitisho hivyo na kusema kuwa anahofia maisha yake.

Decemba mwaka jana Sheikh Idris na mpinzani wake Mohamed Khalifa walinusurika kifo baada ya msikiti wao kuvamiwa na vijana zaidi ya 100, ambao walitawanywa na polisi.

Mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya kumbukumbu ya Pandya, mjini Mombasa

Pamekuwa na matukio ya mara kwa mara ya mauaji ya viongozi maarufu wa dini katika mazingira ya kutatanisha.

R.I.P Sheikh Idris

No comments:

Post a Comment