Na Mwene Said
MSANII
Emmanuel Mbasha (32) ambae ni mume wa Mwimbaji wa Injili, Flora Mbasha
(pichani) akiwa, amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala
akikabiliwa na mashitaka mawili ikiwemo ya ubakaji.
Mshtakiwa huyo ambaye ni mfanyabiashara na mwimbaji alisomewa mashitaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Wilberforce Luago.
Wakili
wa Serikali Nassoro Katuga alidai kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo
mawili maeneo ya Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam.
Katuga
alidai katika shitaka la kwanza kuwa, Mei 23, mwaka huu eneo la Tabata
Kimanga, Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam, kinyume cha sheria huku
akijua ni kosa alimuingilia kwa nguvu msichana anayedaiwa kuwa shemeji
yake (jina limehifadhiwa).
Katika
shtaka la pili, ilidaiwa kuwa Mei 25, mwaka huu eneo la Tabata Kimanga,
jijini Dar es Salaam, kinyume cha sheria, mshtakiwa aliumuingilia kwa
nguvu mfanyakazi wake (jina limehifadhiwa).
Hata hivyo, mshtakiwa alikana mashitaka hayo .
Upande wa Jamhuri ulidai kuwa hauna pingamizi la dhamana.
Hakimu
Luago alitaja masharti ya dhamana kwa mshtakiwa kuwa na wadhamini
wawili, mmoja awe mtumishi wa serikali na mwingine kutoka taasisi
inayotambulika watakaosaini hati ya dhamana ya Sh. milioni 5.
Mshtakiwa
alishindwa kutimiza masharti ya dhamana hivyo alipelekwa rumande na
kesi iliahirishwa hadi Juni 19, mwaka huu itakapotajwa.
Mbasha
akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi alisindikizwa katika basi la
Jeshi la Magereza kwa ajili ya kwenda kuanza maisha mapya katika
mahabusu ya Keko, jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment