Tuesday, June 10, 2014

MH TUNDU LISU AFIKISHA KWENYE JAMII KOMBORA ALILORUSHA MTOTO WA MH JOHN KOMBA LEO 10-6-2014

Hii ni kauli ya Mtoto wa Mbunge wa CCM Captain John Komba aitwaye Gerald John Komba aliyehamia CHADEMA. 

Namnukuu:"Unajua ndugu yangu Mwanahabari, ukiwa Chuoni huwezi kuyaona Maisha halisi ya mtaani, mtaani ndio field kamili na ngumu, lakini ukiwa Chuo tena ukiwa Mtoto wa Kigogo huwezi kuona umuhimu wa kuvi-support Vyama vya upinzani, binafsi nimekwenda Nyumbani Mbinga na Sehemu kadhaa za Nchi hii, hakika Wananchi wanateseka sana". Alisema Gerald ambaye pia Kitaaluma ni Mhitimu wa Shahada ya Sheria ya Chuo Kikuu cha St.Augustine Mwanza. Alipoulizwa na Mwandishi wa habari kama ana mpango wa kwenda kumng'oa Baba yake Jimboni Mbinga kupitia CHADEMA, alisema kwamba hilo lingewezekana endapo angekuwa CCM, lakini kwa CHADEMA hafikirii kama hilo linawezekana kwani CHADEMA hakuna Sera za kurithishana majimbo, huku akitolea mfano wa majimbo ya Chalinze na Kalenga. Pia aliongeza kuwa ameamua kujiunga rasmi CHADEMA, kwa sababu ameona Nchi inapoelekea, ukweli wa mambo unaojulikana unafichwa kwa maslahi ya wachache.

No comments:

Post a Comment