Friday, June 6, 2014

HIVI NDIYO ALIVYOJITETEA MMILIKI WA NYUMBA ALIKOUWAWA NYOKA ANAYEDAIWA NI WA KISHIRIKINA

Mchana wa June 05 kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii zilisambaa taarifa ambazo zilikua zikimhusu mmiliki wa mojawapo ya nyumba maeneo ya Sakina jijini Arusha kuhusu kufuga nyoka ambaye alihusishwa na imani za kishirikina.

CHA2Wananchi walimuua nyoka huyo na kisha kumkata kata vipande,millardayo.com imepata xclusive interview na mmiliki wa nyumba hiyo ambaye kakubali kuelezea kila kitu anachokijua kuhusu nyoka huyo.

Huyu anaitwa Mr.Joseph Paschal Magesa ambaye anaanza kwa kusema>>Mimi kama mimi kwanza ni mkristo safi na mzee wa kanisa sasa mimi nimeondoka jana na mke wangu kutoka arusha kuja Dar es salaam’

‘Sijui lolote kuhusiana na hiko kitu,mimi nimefika hapo katikati ya Mwanga na Same nikapigiwa simu kwamba kuna nyoka huku ndani ya eneo la garden,kuna vijana niliwaacha wawili pale nyumbani nikawaambia waambieni watu wawasaidie kumuua huyo nyoka’

‘Wakamuita jirani yangu hapo ndipo nae akanipigia simu nikamwambia bwana wewe si una bunduki nisaidie kumuua huyo nyoka aliyokata simu nilijua ametekeleza kumbe yeye alikua ameondoka’

‘Baadae napiga tena simu nauliza vipi naambiwa bado yupo na watu wamejaa nikawauliza kwani hao watu hawawezi kumuua mpaka bunduki wakasema wanaweza baadae wakanambia wamemvuta mkia wamemuweka nje ya geti’

‘Nikawauliza anavutika asije akawa analeta shida wakasema anavutika,nikawambia mpelekeni kanisani mimi nipo jirani na kanisa wakamvuta hadi kanisani wakamwagia maji ya baraka kisha wakamkata kata ndo ikawa mwisho wake hapo’.

No comments:

Post a Comment