Monday, June 30, 2014

Hivi ndivyo trend ya #Suarezing ilivyokuwa kubwa mtandaoni.

suarezBaada ya kumng’ata mchezaji mwenzake, Luis Suarez amegeuka kuwa mchezaji anayetrend sana au anayezungumziwa sana kupitia mtandao wa Twitter kwa kutumia hashtag ya #Suarezing huku ikiambatana na picha mbalimbali zilizotengenezwa za kumtania mchezaji huyo kwa kitendo alichofanya.
suarez3Tangu mchezaji huyo wa Uruguay apewe adhabu ya kufungiwa kwa kumng’ata mchezaji wa Italia Giorgio Chiellini amekuwa akimake headlines kila kukicha katika mitandao haswa Twitter.
suarez2Ilianza kama utani tu kwa watu kutengeneza picha lakini sasa kimegeuka kuwa kitu kikubwa huku wengine wakijipiga picha hata barabarani kuiga kitendo kilichofanywa na Suarez wakati wa moja ya mechi za kombe la dunia.

No comments:

Post a Comment