Tuesday, April 15, 2014

MSD YATOA TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UTENDAJI NA MIPANGO YAKE

Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda na Huduma kwa Wateja Bohari ya Dawa (MSD), Edward Terry, akizungumza na waandishi wa habari.
Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda na Huduma kwa Wateja Bohari ya Dawa (MSD), Edward Terry, akizungumza na waandishi wa habari.
Ads by OnlineBrowserAdvertisingAd Options
Mkurugenzi wa Manunuzi wa MSD, Heri Mchunga akiwa katika mkutano huo.
Ofisa Habari wa MSD, Etty Kusiluka akiwa katika mkutano huo.
Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda na Huduma kwa Wateja Bohari ya Dawa (MSD), Edward Terry (katikati), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu Utendaji na Mipango ya MSD. Kushoto ni Mkurugenzi wa Manunuzi wa MSD, Heri Mchunga na Ofisa  Idara Habari Maelezo, Frank Mvungi. 
Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda na Huduma kwa Wateja Bohari ya Dawa (MSD), Edward Terry (kulia), akizungumza na wanahabari. Kushoto ni Mkurugenzi wa Manunuzi wa MSD, Heri Mchunga.
Mkurugenzi wa Manunuzi wa MSD, Heri Mchunga, akizungumza na wanahabari kuhusu utaratibu wa kununua dawa na vifaa tiba kutoka nje ya nchi. Kulia Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda na Huduma kwa Wateja Bohari ya Dawa (MSD), Edward Terry .
Ads by OnlineBrowserAdvertisingAd Options
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

BOHARI ya Dawa (MSD) imesema asilimia 80 na asilimia 95 ya dawa na vifaa vya tiba  huagizwa toka nje ya nchi. 

Kauli hiyo imetolewa leo jijini  Dar es Salaam na  Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda na Huduma kwa Wateja Bohari ya Dawa (MSD), Edward Terry , alipokuwa akielezea kuhusu utendaji na mipango ya bohari ya dawa (MSD).

Terry alisema bohari ya dawa ipo chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii iliyoundwa kwa mujibu wa sheria namba 13 ya mwaka 1993 na inajiendesha chini ya bodi ya wadhamini. 

Alisema kuwa Bohari ya Dawa MSD ina jumla ya kanda tisa nazo ni Mwanza, Tabora, Mbeya, Iringa, Dodoma, Tanga, Moshi, Mtwara na Dar es Salaam pia ili kuendelea kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi imefungua kituo kingine wilayani Muleba mkoani Kagera mwezi machi mwaka huu.

Hata hivyo alisema majukumu ya msingi ya bohari ya dawa   ni kununua, kuhifadhi na kusambaza dawa, vifaa vya tiba na vitenganishi vya maabara kwenye hospitali, vituo vya afya na zahanati za umma pamoja na taasisi zilizoidhinishwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

"Upatikanaji wa dawa umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka kulingana na bajeti ya serikali na katika ziara ya kamati ya kudumu ya bunge ya huduma za jamii katika mkoa wa Mtwara ya kuangalia upatikanaji wa dawa na vifaa tiba mwezi Februari mwaka huu ulionyesha kuwa hali ya upatikanaji wa dawa katika Hospitali za Wilaya ya Masasi imefikia asilimia 90,"

Bohari ya Dawa (MSD) hununua dawa na vifaa tiba kwa kuzingatia miongozo ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii pia lazima visajiliwe na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) wakati vitenganishi vya maabara husajiliwa na kuidhinishwa na Private Health Laboratories Board(PHLB).

Kabla ya kuruhusu dawa, vifaa na vitenganishi vya maabara kuingia nchini  hukaguliwa  na kupimwa kwa ushirikiano wa taasisi za serikali kama Tanzania Bureau Agency (TBS),  Tanzania Government Chemist Laboratory Agency (GCLA) na The Bureau  Industrial Cooperation (BICO).

Terry alisema mwaka 2010 MSD ilifanya jaribio la kwanza la kufikisha dawa moja kwa moja katika vituo vya afya na hatua hii ilitokana na agizo la Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambapo zoezi hilo lilifanyika katika kanda ya Tanga.

"Jaribio la kwanza lilifanikiwa kwa kiasi kikubwa na kupelekea mnamo mwaka 2011-2012 mikoa mingine tisa kuingizwa katika utaratibu wa kufikisha dawa na vifaa tiba moja kwa moja hadi hospitali, vituo vya afya na zahanati".

Alitaja mikoa hiyo kuwa ni Shinyanga, Lindi, Dodoma, Kigoma, Manyara, Rukwa, Pwani, Ruvuma na Dar es Salaam na pia kuanzia julai 2013 mpango huu  wa utoaji huduma katika vituo vyote ulienezwa nchi nzima.

Terry alifafanua kuwa MSD ni kitengo cha Serikali cha mikakati ambacho wakati wote kiko tayari kukabiliana na majanga yanapotokea nchini na bohari ya dawa kwa kushirikiana na wahisani inaendelea na mpango wa kupanua maghala ili kuongeza nafasi za kuhifadhi dawa na vifaa tiba.

Hata hivyo alitaja changamoto zinazoikabili bohari ya afya kuwa ni udokozi wa dwa unaofanywa na wafanyakazi wasio waaminifu, uhaba wa viwanda vya dawa na tiba nchini, baadhi ya vituo vya afya kutoleta maombi ya dawa  na vifaa tiba katika kanda za MSD kwa wakati, fedha kutoka hazina kuja MSD kutofika kwa muda muafaka ikiwemo ongezeko kubwa la mahitaji kulinganisha na uwezo wa serikali.

Hata hivyo Terry aliotoa onyo kwa wafanyakazi waliopo kwenye vituo vya huduma ya afya kuacha mara moja tabia ya udokozi wa dawa ili kuboresha upatikanaji mzuri wa dawa kwa wagonjwa katika vituo hivyo vya afya.


No comments:

Post a Comment