Monday, April 14, 2014

MKUU WA MKOA WA ARUSHA AZUNGUMZIA TUKIO LA BOMU KULIPUKA KWENYE BAA USIKU APRILI 13, 2014

    

Usiku wa April 13 2014 kwenye baa iitwayo ‘Arusha night park’ iliyopo Mianzini Arusha ambayo siku zote ni miongoni mwa sehemu zinazokua na mkusanyiko wa watu wengi kuanzia jioni, limerushwa bomu wakati watu mbalimbali wakitazama mpira.Blog
hii imepata nafasi ya kuongea na mkuu wa mkoa wa Arusha ambae ni
kiongozi  wa Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa ambae amethibitisha
kwamba ni  watu 15 wamejeruhiwa kwenye mlipuko huo.

Anasema  wote wamepelekwa hospitali ambapo uchunguzi wa awali
umeonyesha bomu  hilo ni la kutengenezwa kwa mkono na mpaka sasa
hajajulikana  alietekeleza shambulio hilo.

Kwenye sentensi nyingine pia amesema hakuna aliepoteza maisha kwenye shambulio hilo ambalo uchunguzi wa awali umeshatoka, ila baadae itatoka taarifa rasmi pale uchunguzi kamili utakapokamilika.
>>>millardayo.com

No comments:

Post a Comment