Friday, March 21, 2014

WAKATI WASANII WAKIMSUJUDIA JIJINI DAR OSTAZ JUMA AIBU MBAYA HUKO KWAO MUSOMA, AMTELEKEZA BABA YAKE MZAZI MAISHA ANAYOISHI YANASIKITISHA SANA..!!

 

 

 

 







Mdau wa muziki wa kizazi kipya na bingwa wa kejeli kwa wasanii na waandishin wa habari Juma Ibrahim almaarufu Ostaz Juma na Musoma ameumbuka!


Hiyo inatokana na hivi karibuni timu ya mtandao huu iliamua kufunga safari hadi kijijini Majita Musoma kwa baba mzazi wa Ostaz Juma na Musoma na kushuhudia maisha ya familia yake yalivyo. Safari hiyo ilichangiwa na mambo mawili makuu, moja, mtandao huu ulipokea malalamiko toka kwa wakazi wa kiji cha Majita huko Musoma alikokulia Ostaz Juma kwamba wanashangazwa kusikia Ostaz Juma akiimbwa katika bendi nyingi za muziku huku akitukuzwa kama mfalme au Pedeshee
Pia wakasoma katika magazeti kwamba kuna msanii aliyepigwa picha na Ostaz Juma akimpigia magoti akimbembeleza amsamehe kwa aliyomkosea jambo ambalo kibnadamu liliwakera wengi kutokana na kuwa na hisia za udharilishaji


kutokana na malalamiko hayo mtandao huu ulimfikishia ujumbe Ostaz Juma kwa njia ya simu lakini kutokana na upeo mdogo wa akili wa Ostaz Juma alianza kutukana na kumtishia kumchinja mwandishi aliyempigia simu huku akijigamba kuwa yeye ni mkulya na kuchinja watu ni kawaidia ya kabila hilo


Hapo ndipo ilipoibuka sababu ya pili ya mtandao huu kuamua kupanga safari na kwenda kijiji kwa baba yake na Ostaz juma , haikuwa kazi rahisi kufika lakini kutokana na majukumu ya kazi ilibidi kwenda tu.

Baba wa ostazi Juma akiongea kwa uchungu
Majira ya saa moja na nusu asubuhi siku ya jumanne ya wiki hii waandishi wetu waliondoka Musoma mjini kuelekea kijijini Mjita wakitumia usafiri wa basi unaotumia na wananch wa eneo hilo mpaka kufika home kwa mshua wa Ostaz Juma na Musoma

 baada kuliza watu wachache tulielekezwa mzee huyo anaonekana ni maarufu sana kutokana jina lamwanae kusikika likipaushwa kwenye mabendi na kuandikwa kwenye magazeti aibu ya kwanza kushudiwa ilikuwa ni makazi duni ya familia ya akina ostaz juma ambae jijini anafahamika kama pendeshee nyumba kazaa chakavu zilizojengwa kwa udongo na kuezekwa kwa bati za kuunga unga na nyasizinaonekana kwenye kwenye makazi ya mzee Iblahim nyumba moja tu ndo ilionekana kujngwa kwa tofari kuu kuu ambazo haikujulikana zimetumia mchanga gani huku sehemu pekee ya kifahari katika eneo hilo ikionekana ikionekana ni uzio wa waya (kama ule uwekwao kwenye mabanda ya kuku) ulionunuliwa na ostaz juma na kuzungushiwa katika makaburi kumi ya familia hiyo baada ya kubisha hodi kwa muda alijitokeza mwanadugu mmoja alipoulizwa mahali mzee mwenye mji alipo alijibu mzee hayupo ameenda kwa mganga kutibiwa mguu unamsumbua sana lakini siyo mbali sanaa toka hapa mtandao huu uliamua kumfuata mzee ibrahim  na kuhojiana nae
Baba Mzazi wa Ostaz Juma akielezea mabaya ya mwanae


Mwandishi-shikamoo  mzee Ibrahim pole kwa maradhi 
Mzee Ibrahim -asante sana ningependa kufahamu nyie ni wageni wangu toka wapi 

Mwandishi - sisi tunatoka dar es salaam ni jamaa zake na ostaz juma Mzee Ibrahim - oh karibuni sana wanangu nimefurahi sana  kunitembelea niko hapa na kula dawa maana mguu unanisumbua sanaa 

Mwandishi- pole sana baba mungu atakujalia utapona baada ya kukaribishwa na kuongea machache mzee ibrahim alitutaka twende tukapaone nyumbani kwake tulipofika mazongumzo yaliendelea 

Mwandishi - hivi ostaz juma anataarifa za wewe  kuumwa mguu 

Mzee ibrahim- azipate wapi wanangu Juma amehalibikiwa na mkewe aitwaye Mariam hatujari kabisa wala hatusaidii  kwa chochote zamani alikuwa na mke mwingine alikuwa na roho nzuri sana wadogo zake wamefukuzwa shule kwa kukosa ada nimepiga naye kelele kazi yake ni kutunza mji wa ukweni na kutafuta sifa huko mjini sijui amekuwa je maana sikuzaa watoto wajinga mimi kuna siku alikuja hapa na yule kijana  anaeitwa abubakari sadiki(mtangazaji  wa radio one)nikamuuliza na wewe kwenu pako hivi akainama chini kwa aibu akaondoka na kwenda gest kulala lakini baadae alikuja na kuniambia atazungumza nae akusaidia  kwani hata mimi ananisaidia sana huyu jamaaa 

Mwandishi - kwanini ana kuwa hodari wa kusaidia watu halafu wewe mzazi wake hakujari 
Nyumbani kwa akna Ostaz Juma na musom


Mzee Ibrahim - tena afadhari yangu  mimi mama yake mzazi yuko mwanza huyo ndo hafaidiki na chochote  kutoka kwa Ostaz Juma huyu mama mnaemuona hapa ni mama yake wa kambo ndiye aliyemlea toka mdogo alikuwa akimfulia adi kaptura zake za mkojo mpaka akakuwa ni mama  ni mama mzuri sana kwa sababu alimlea kwa mapenzi ya haliya juu sana 

 Mwandishi-  niujumbe gani ungependa tumfikishie tutakaporudi dar es salaam 

Mzee Ibrahim- mwambieni awakumbuke wadogo zake kwani akishindwa kuwasaidia  hawa nani atakayewasaidia ? itafikia siku mimi ntakufa na yeye atakufa sasa hawa tuliowaacha watajivunia nini ikiwa tumeshindwa  hata kuwasomesha

No comments:

Post a Comment