Hatimaye
aliyekuwa Mwenyekiti wa muda Bunge Maalum Pande Ameir Kificho leo
ameachia wadhifa wa kiti hicho na kumkabidhi jukumu hilo Mwenyekiti wa
bunge hilo la katiba Samwel Sitta na Makamu wake Samia Suluhu Salehe ili
kuongoza mchakato wa kuijadili rasimu ya katiba.katiba mpya itakayowaondolea umaskini wananchi huku ikidumisha Muungano wa Tanzania unaotimiza miaka 50 mwaka huu.
Baada ya kukalia kiti hicho, SITTA ametumia fursa hiyo kushukuru utendaji wa mwenyekiti wa muda na kuwataka wajumbe kuanza kufuata kanuni zilizopitishwa na bunge hilo na kwamba hatosita kumchukulia hatua mjumbe atakayeenda kinyume na taratibu zilizopo.
Baada ya tamko hilo kazi ya kuanza
kuwaapisha wajumbe ilianza huku Mwenyekiti Mstaafu PANDU AMEIR KIFICHO
akifungua pazia la zoezi hilo litakalofanyika mfululizo kwa siku tatu.
No comments:
Post a Comment