Wednesday, March 5, 2014

MTOTO ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUCHINJWA NA BABA YAKE HUKO KAHAMA,KISA KUUGUA MUDA MREFUMtoto Said Siraji akiwa amelazwa katika Hospital ya wilaya ya Kahama
Mtukio ya kikatili yameendelea kushika kasi wilayani Kahama mkoani Shinyanga ambapo mtoto aitwaye Said Siraji/Said Joshua  amelazwa katika Hospitali ya wilaya usiku wa kuamkia leo, baada ya kunusurika kifo katika jaribio la kuchinjwa na baba yake mzazi aliyejulikana kwa jina la Salvatory. 
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya wilaya-Kahama; Dakta Joseph Fwoma amesema Siraji amefikishwa hospitalini hapo leo alfajiri baada ya kuokotwa na wasamaria wema akiwa anakimbia huko akivuja damu shingoni. 
Dakta Fwoma amesema baada ya kufikishwa hospitalini madaktari walimfanyia upasuaji na kumshona sehemu ya koromeo aliyochinjwa na hadi alasiri hii hali yake imeendelea vizuri hasa baada ya kuongezwa damu

No comments:

Post a Comment