Stori: Gladness Mallya
STAA wa filamu za Kibongo, Ruth Suka ‘Mainda’ amejikuta akikumbuka pete aliyovishwa na aliyekuwa mchumba wake, marehemu Saidi Banda ‘Max’ na kusema ataendelea kumuombea kwani alikuwa ni mwanaume aliyekuwa na malengo makubwa kwake.
Mainda alifunguka hayo kupitia mtandao mmoja wa kijamii na kusema kuwa kila akiziona picha za siku alipovishwa pete ya uchumba, anajikuta akitokwa na machozi.
“Miaka inakimbia sana miss u so much...! Kama ndoto vile, siku ile sitaki kuikumbuka ila kwa yote namshukuru Mungu.
“Asante
Saidi kwa sababu ulionyesha kuwa una malengo makubwa na mimi mpaka
sasa ningekuwa naitwa Mrs, upendo wako kwangu bado upo sanaa ila hilo
ulilolianzisha kwenye kidole changu japo ndoto haikukamilika kupitia
wewe litatendeka, asanteni wote mlioshiriki siku ya hili tukio akiwemo
Nina na Dotnata,” aliandika Mainda.
STAA wa filamu za Kibongo, Ruth Suka ‘Mainda’ amejikuta akikumbuka pete aliyovishwa na aliyekuwa mchumba wake, marehemu Saidi Banda ‘Max’ na kusema ataendelea kumuombea kwani alikuwa ni mwanaume aliyekuwa na malengo makubwa kwake.
Mainda alifunguka hayo kupitia mtandao mmoja wa kijamii na kusema kuwa kila akiziona picha za siku alipovishwa pete ya uchumba, anajikuta akitokwa na machozi.
“Miaka inakimbia sana miss u so much...! Kama ndoto vile, siku ile sitaki kuikumbuka ila kwa yote namshukuru Mungu.

No comments:
Post a Comment